WANAFUNZI WA UDAKTARI UDOM WAANZA MAFUNZO KWA VITENDO NZEGA


  • 13 days ago
  • School of Medicine and Dentistry

Siku ya leo tarehe 19/5/2023 wanafunzi wa Udaktari mwaka wa Tatu Çhuo Kikuu cha Dodoma Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa wameanza mafunzo kwa vitendo ya wanafunzi yaani CDC field (Communicable Disease Control) Kuzuia Magonjwa ambukizi na viashiria vyake katika jamii

Dhamira ya mafunzo haya ni kuelimisha na kujua kiwango cha maambukizi ya minyooo ya tumbo(Interstinal infestation worms infestational ) kwa watoto wenye umri wa miaka 3 hadi 12,waishio halmashauri ya Nzega Mkoani Tabora

Timu ya madaktari na wanasayansi wa maabara kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na wanafunzi wa udaktari UDOM watatembelea halmashauri ya mji wa Nzega mkoa wa Tabora, zoezi hili litafanyika kwa muda wa siku 10 ambapo inategemewa watoto zaidi ya 6,000 kufikiwa

Taarifa kadhaa katika jamii zitachukuliwa pamoja na kupimwa choo kikubwa ili kudhibitisha kiwango cha maambukizi katika kata hizo na elimu ya afya itatolewa kwa jamii halmashauri ya wilaya Nzega

Waratibu wa zoezi hili la mafunzo kwa vitendo wametembelea ofisi mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya nzega zikiwemo ofisi ya mkuu wa wilaya,ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega ,ofisi za watendaji wa kata mbalimbali na Kituo cha polisi ili kufuata taratibu mbalimbali.

UDOM TUNAJIFUNZA KWA VITENDO ZAIDI
 

Comments
Send a Comment