KAMATI YA BARAZA YA MILIKI YATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO UDOM


  • 1 month
  • The University of Dodoma

Kamati ya Baraza ya Miliki ya Chuo Kikuu cha Dodoma, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Chuo ikiwemo ukarabati wa nyumba za wafanyakazi, ujenzi wa Kituo cha Mionzi katika hospitali ya Chuo pamoja na shule ya Msingi ya Mfano Chimwaga.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa muda wa Kamati hiyo Dkt. Saitori Laizer, amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Chuo katika maeneo mbalimbali hususani katika Hospitali, pamoja na kuhimiza Menejimenti ya Chuo kuweka mpango thabiti utakaowezesha kufanikisha ukarabati wa nyumba za wafanyazi zilizopo Kisasa nyumba 300 na Njendengwa, ili ziendane na hadhi ya Chuo.

Comments
Send a Comment