UDOM KIVUTIO UZALISHAJI BIDHAA ZA CHAKULA


  • 3 weeks
  • School of Nursing and Public Health

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Angellah Kairuki  (Mb) amewaelekeza wadau kuunga mkono jitihada za Chuo Kikuu cha Dodoma katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za Chakula.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo alipotembelea Banda la UDOM Jumanne tarehe 29, Agosti 2023 wakati wa Mkutano wa Tathmini ya Mkataba wa Lishe kati ya Mhe. Rais na wakuu wa Mikoa lililofanyika katika Mji Mkuu wa Serikali Mtumba- Dodoma

Aidha, ametoa pongezi kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kazi kubwa inayofanywa hususani kwenye uzalishaji wa Makao ya Chakula na Lishe.

Katika maonesho hayo, Chuo Kikuu cha Dodoma kimeshiriki kwa kuonesha bunifu mbalimbali zinazofanywa na wakufunzi pamoja na Wanafunzi wanaosoma Programu ya Afya na lishe “Clinical Nutrition and Dietetics”

Comments
Send a Comment