WAFANYAKAZI UDOM WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI DODOMA


  • 8 months
  • The University of Dodoma

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka wameshiriki Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kimkoa imefanyika katika Viwanja vya Jamhuri Dodoma.
Sherehe hizo ambazo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ziliongozwa na kauli mbiu isemayo "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Naisha".

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii Prof. Razack Lokina, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Comments
Send a Comment