UDOM-SoNPH WATOA HUDUMA KWA JAMII WILAYANI CHEMBA


  • 11 days ago
  • School of Nursing and Public Health

Amidi wa Shule kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii Dkt. Stephen Kibusi leo tarehe 21/5/2023 ameongoza zoezi la kutoa huduma kwa jamii wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma kwa kupima wananchi magonjwa yasiyoambukiza yaani Shinikizo la Damu ( Blood Pressure), kisukari na kutoa ushauri kwa jamii ikiwa ni kurudisha kwa jamii kama jukumu mojawapo la Chuo Kikuu cha Dodoma

Pia viongozi, wahadhiri pamoja na wanafunzi wa Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya jamii waliweza kutembelea vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Chemba, kalema,Gwandi, Chambalo, Goima na Kidoka

Comments
Send a Comment