UDOM YASHIRIKI KIVITENDO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


  • 3 weeks
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) ni miongoni mwa Taasisi za Umma zinazoshiriki kivitendo maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park Dodoma.

Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene alipotembelea maonesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Bi. Rose Joseph, amesema UDOM katika Banda lake imejikita kutoa huduma zifuatazo: Upimaji wa Afya bure na ushauri wa kiafya kwa wananchi, kufanya matengenezo ya simu za mkononi na komputa zilizoharibika bure, huduma ya msaada na ushauri wa kisheria bure, pamoja na elimu ya jumla kuhusu Mafunzo, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu unaotolewa na Chuo hicho.

Waziri Simbachawene ameipongeza UDOM kwa jitihada hizo za kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo yanayoendelea hadi Jumapili tarehe 23 Juni 2024.
 

Comments
Send a Comment