MTENDAJI MKUU WA BENKI YA NMB ATEMBELEA UDOM


  • 9 days ago
  • Office of The Vice Chancellor

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania  Bi.Ruth Zaipuna ametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma tarehe 19 Mei, 2023 kwa lengo la kuzungumza na Chuo kuhusu fursa mbalimbali za benki ya NMB.

Fursa hizo ni pamoja na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka alimshukuru sana Bi. Ruth Zaipuna kwa kushirikisha Chuo Kikuu cha Dodoma fursa mbalimbali zinazipatikana katika Benki ya NMB na kwamba Chuo kitazifanyia kazi.

Mtendaji Mkuu wa NMB aliambatana na viongozi mbalimbali wa benki hiyo wa ngazi ya tawi, mkoa, kanda na makao makuu

Comments
Send a Comment