MIAKA MITANO YA HUDUMA ZA KUPANDIKIZA FIGO
Siku ya leo tarehe 13/3/2023 Hospitali ya Benjamin Mkapa(BMH), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Tokushukai Medical Group wameadhimisha miaka mitano tangu kuanzisha huduma za kupandikiza figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa
Wakati wa kuelezea mafanikio ya Miaka mitano ya Upandikizaji Figo Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema " tumefanikiwa kupandikiza wagonjwa thelathini na tatu (33) kati ya hawa, wagonjwa ishirini na mbili (22) walipandikizwa figo na watalaamu wazawa. Ni furaha yangu kuwaambia kwamba kwa sasa wataalamu wetu wanafanya zoezi hili wao wenyewe bila ya kuwepo kwa usimamamizi wa watu wa Japani"
Mwenyekiti wa Tokushukai Medical Group Dkt.Higashiue Shinichi ameaahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Japani na kuwa wanampango wa kujenga kituo kipya kama kumbukumbu kwao na ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya kwa Upandikizaji figo kwa wanafunzi
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoitangaza nchi na kuwa ipo siku watu toka nchi nyingine watakuja kujifunza upandikizaji wa figo Tanzania
Aidha Prof. Kusiluka amesema "kwa kazi nzuri ambayo imeanza na watangulizi wetu, mimi kama Vice Chancellor wa Chuo Kikuu cha Dodoma na wenzangu tutakuwa ni wa ajabu sana kama tutairudisha nyuma hii shughuli, kwa hiyo tunaahidi kwamba tutaendeza hii kazi kwa pamoja na Hospitali ya Benjamin Mkapa na wadau wetu"