UDOM YAENDESHA MAFUNZO KWA WAELIMISHA RIKA


  • 2 days
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tarehe 21 Mei, 2025 kimeanza mafunzo ya siku tano kwa Waelimishaji Rika 104 (Peers Educators) .

Mafunzo hayo yanayofanyika katika Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii yanalenga kuwajenga vijana washiriki kimaarifa, ujuzi, na maadili mema ili waweze kuwa mabalozi wazuri pamoja na kuwa waelimishaji mahiri katika kuwawezesha vijana wenzao kufanya maauzi yenye tija kiafya na kielimu.

Mafunzo hayo ni katika kutekeleza ahadi iliyotolewa na Naibu Makam Mkuu wa Chuo-Taalumu, Utafiti, na Ushauri elekezi, Prof. Razack Lokina wakati wa kufunga mafunzo kama hayo mwaka 2023 chini ya Mradi wa UNESCO wa O3 Plus.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma Bi. Rhoda Aroko, amesema chuo kimeona mchango wa waelimishaji rika ndio maana kimekuwa tayari kuendeleza mafunzo hayo, pia alisisitiza washiriki kujituma wakati wote wa mafunzo kwani wanategemewa kuwa kiungo muhimu kati ya watoa huduma na wanafunzi.

"Niwaombe sana muwe wahudhuriaji na wasikivu wazuri wa mafunzo haya kwani yatawabadilisha ninyi na kuwapa nafasi ya kuboresha utendaji kazi wenu pamoja na CV zenu" Alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi, Mratibu wa Mradi wa UNESCO wa O3 Plus kwa Dodoma, Bw. Faraja Msangi alisema UNESCO inatambua na kushukuru jitihada kubwa zinazofanywa na uongozi wa UDOM wa kuendeleza matokeo ya mradi ikiwemo programu ya waelimishaji rika na kuahidi kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi kwa karibu na chuo katika kuendeleza matokeo chanya ya mradi chuoni.

Comments
Send a Comment