MKUTANO KATI YA MENEJIMENTI UDOM NA WAFANYAKAZI
Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), leo tarehe 21 Mei, 2025 imefanya mkutano na Wafanyakazi uliolenga kujadili maendeleo ya UDOM pamoja na kujadili changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua.
Mkutano huu uliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, na kuhudhuriwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Albino Tenge na Menejimenti yote ya UDOM