UNESCO YATIMIZA AHADI YAKE UDOM


  • 1 year
  • Directorate of Students Services

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Mradi wake wa O3 PLUS ambao unatekelezwa kwenye vyuo 15 hapa nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma, leo tarehe 13 April 2023 limeanza mafunzo kwa waelemishaji rika 40 kwa Chuo Kikuu cha Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi walioitoa wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kundi la kwanza la waelemishaji rika 80 mwezi Januari, 2023.

Mafunzo haya yanafanyika kuanzia leo tarehe 13 hadi tareh 18 Aprili 2023 na yanakifanya Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa na waeleimshaji rika waliopata mafunzo kutoka UNESCO kufikia 120 ambao wanajukumu la kuwa mabalozi wazuri pamoja na kuwasaidia vijana wenzao katika kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo mimba zisizotarajiwa, maambukizi mapya ya VVU pamoja na Ukatili wa kijinsia.

Itakumbukwa kwamba wakati wa kufunga mafunzo kwa waelimishaji rika 80 mnamo tarehe 2 mwezi Januari, 2023 mbele ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Razack Lokina, UNESCO waliaahidi kuongeza idadi ya waelimishaji rika kutokana na ukubwa wa Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na mwiitikio mkubwa uliooneshwa na vijana kutaka kuwa waeleimshaji rika.

Kutimia kwa ahadi hiyo kunaongeza nafasi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kupata taarifa na dondoo muhimu zinazoweza kuwasiadia kutimiza malengo yao. Hivyo vijana wameaswa kuwatumia waelimishaji rika hao katika kupata taarifa na ushauri muhimu kuhusu changamoto wanazopitia

#Kijana Elimika, Elimisha Wengine

Comments
Send a Comment