MAFUNZO KWA WAELIMISHAJI RIKA UDOM YAMALIZIKA
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia mradi wake wa O3 PLUS, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma, wamehitimisha mafunzo kwa waelimishaji rika wapatao 40. Kukamilika kwa mafunzo hayo kunaifanya UDOM sasa kuwa na waeleimishaji rika wapatao 120 ambao wanategemewa kuwafikia vinaja wenzao zaidi ya 10,000.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoanza tareh 13 na kukamilika leo tarehe 18/4/2023, Bi. Rhoda Aroko, Mkurugenzi wa huduma za wanafunzi aliwashukuru UNESCO kwa kuja na program hii na kusistiza kuwa UDOM ipo tayari wakati wowote kushirikiana na UNESCO pamoja na wadau wengine katika kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao.
Akizingumza hapo awali kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Bw. Ngalula Jackson alishukuru kwa mafunzo na kukiri kuwa yamekuwa na tija kwao binafsi pamoja wataenda kugusa maisha ya vijana wenzao.
" Tumeelimika, tunaelimisha wengine, njoo tuzungumze"