WARSHA YA KUWAONGEZEA UJUZI WASIMAMIZI WA WANAFUNZI WA SHAHADA ZA JUU


  • 1 year
  • Directorate of Postgraduate Studies

Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma Profesa Lughano Kusiluka ametoa wito kwa wasimamizi wa wanafunzi wanaosoma Shahada za Juu kuitumia vema warsha ya kuwaongezea ujuzi iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Shahada za Juu ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kufanyika leo tarehe 03/05/2023 katika Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Profesa Razack Lokina amesema ni matumaini yake kuwa warsha hii italeta tija kwa pande zote mbili, yaani wasimamizi na wanafunzi kwa ujumla katika kuhakikisha wanafunzi wanamalizia masomo yao kwa wakati.

Warsha hiyo ilihusisha pia wahadhiri kutoka nje ya UDOM akiwemo Profesa Esron Karimuribo kutoka chuo cha kilimo Sokoine (SUA) cha Morogoro pamoja na Profesa Karim Manji kutoka (MUHAS)
 

Comments
Send a Comment