WAHITIMU WAJITOKEZA KWA WINGI KUTEMBELEA BANDA LA UDOM
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wamejitokeza kwa wingi kutembelea Banda la UDOM katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa SABASABA, ambapo kuna dawati maalum la kuwahudumia wahitimu. Pamoja na huduma nyingine, wahitimu wamepata fursa ya kupatiwa maelezo juu ya shughuli za maendeleo ya Chuo ili kuwapa fursa ya kushiriki katika kukiendeleza Chuo chao.
Akizungumza katika mahojiano na wanahabari, mmoja wa wahitimu hao ndugu Karimu Meshack ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko na Shirika ya Bima la Taifa NIC ameeleza kuwa elimu aliyoipata Chuo Kikuu cha Dodoma imemsaidia katika kulitumikia taifa kwa nafasi aliyo nayo sasa lakini pia kupata kipato cha hudumia familia yake na jamii kwa ujumla. Ndugu Meshack ameupongeza uongozi wa Chuo kwa kuweka utaratibu wa kuwatambua wahitimu na kuwapa taarifa mbalimbali za Chuo. Ametumia fursa hiyo kuwaalika watimu wote wa UDOM kutemblea banda ya Chuo Kikuu cha Dodoma ili waweze kupatiwa taarifa mbalimbali za maendeleo ya Chuo.
Pamoja na kupatiwa taarifa za Chuo wahitimu pia wanapewa zawadi maalum za WAHITIMU UDOM kama kumbukumbu yao na kusaini kwenye bango la wahitimu lililopo katika banda hilo.