VIONGOZI UDOSO WATAKIWA KUWA KIPAUMBELE KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI
Rasi wa Ndaki ya insia na Sayansi za Jamii Prof. Albino Tenge, amewataka Viongozi wa serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma, kuwa kipaumbele cha kutatua Changamoto za wanafunzi pindi zinapotokea kwa kufuata utaratibu
Prof. Tenge ameyasema hayo kwa niaba ya Makamu Mkuu Chuo katika ufunguzi wa Semina ya viongozi wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika tarehe 15 Julai 2023 iikihusisha viongozi wa serikali ya wanafunzi toka Ndaki, Shule kuu na Taasisi zilizopo chuoni hapa.
Prof. Tenge amesema "baada ya semina hiyo anategemea mabadiliko makubwa katika namna wanavyoshughulikia changamoto mbalimbali na jinsi ya kuzitatua, kama viongozi.
“Chuo Kikuu cha Dodoma tunasema kwamba tunaamini changamoto zote zinatatuliwa kwa majadiliano na hatutegemei nyie viongozi wa serikali ya wanafunzi kuwa chanzo cha migogoro” alisisitiza.
Semina hiyo ya siku mbili ililenga kuwajengea uwezo wa uongozi Viongozi wa wanafunzi ili wawe viongozi wenye maadili na wawajibikaji kwa maendeleo ya Chuo na Taifa kiujmula.