KASI YA UKUAJI UDOM YAWAVUTIA WANANCHI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA)


  • 1 year
  • Directorate of Research, Publications and Consultancy

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Wineaster Anderson, amefurahishwa na mahudhurio ya Wananchi wanaotembelea Banda la maonyesho Sabasaba, akiamini kasi ya ukuaji wa UDOM ndiyo kichocheo cha wananchi wengi kutembelea banda hilo.

Prof Anderson ameyasema hayo alipotembelea banda la UDOM tarehe 7 Julai, 2023 katika maonyesho ya 47 ya Kimataifa SABASABA yanayoendelea katika viwanja vya Mwl Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Prof. Anderson amesema kwa sasa uongozi umejizatiti kuhakikisha inaongeza ubora wa huduma, ili kuwavutia wananchi wengi zaidi kujiunga na chuo hicho chenye zaidi ya programu 80 za mafunzo katika fani mbalimbali. Ameongeza kuwa lengo la UDOM ni kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Bora barani Afrika.

Amewataka Wananchi kutembelea kwa wingi kwenye Banda la maonyesho la UDOM ili kujionea bunifu, tafiti na programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.

Banda UDOM limewavutia wadau wengi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wanaoamini kwenye tafiti na matokeo yanayotokana na tafiti kwenye bidhaa na uwekezaji. Aidha, wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Vyuo Vikuu ni miongoni mwa wateja wanaotembelea banda la UDOM kwa wingi.

Comments
Send a Comment