UAPISHO WA VIONGOZI WATEULE UDOSO 2023/24


  • 1 year
  • Directorate of Students Services

Siku ya leo tarehe 31/5/2023 umefanyika uapisho wa viongozi wateule Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma 2023/24 ngazi ya Uraisi, Makamu wa Rais, Magavana, Manaibu Gavaba, Spika, Naibu Spika pamoja na Katibu wa Bunge; Uapisho huo umefanyika katika Jengo la Benjamin Mkapa Ukumbi wa Baraza la Chuo

Akizungumza wakati wa Uapisho huo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka amewapongeza viongozi wote waliomaliza muda wao kwa uongozi uliotukuka. Aidha, aliwapongeza viongozi wapya kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Wanafunzi wenzao na amesisitiza watumie nafasi zao vizuri na kuwahakikishia kuwa Menejimenti ya Chuo itawapa ushirikiano wowote wanaohitaji

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii Prof. Razack Lokina amewataka viongozi wote waliochaguliwa kuzingatia masomo kwani pamoja na kuwa ni viongozi wasisahau uanafunzi wao

Aidha Naibu Makamu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof.Wineaster Anderson amewataka viongozi wote waliochaguliwa waongoze kwa kwa kufuata Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo yote iliyopo
 

Comments
Send a Comment