MAFUNZO YA UONGOZI UDOSO 2023/24 YAKAMILIKA PWANI-KIBAHA


  • 1 year
  • Directorate of Students Services

Mafunzo ya uongozi kwa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOSO 2023/24) yamekamilika tarehe 3 Juni 2023 katika Shule kuu ya Uongozi ya Mwl.Julius Nyerere Kibaha-Pwani.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo na utoaji wa vyeti Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof.Lughano Kusiluka aliwataka viongozi kwenda kuyaishi yale yote waliyofundishwa; Prof Kusilika allieleza kuwa wameaniniwa ndio maana wamechaguliwa hivyo aliwahimiza kwenda kuongoza vizuri kulingana na sifa za kiongozi bora.

Makamu Mkuu wa Chuo pia alimpongeza Mkurugunzi wa Huduma kwa Wanafunzi Bi. Rhoda Aroko na timu yake kwa kuwalea Wanafunzi vizuri.

Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo alimpongeza Rasi wa Shule kuu ya Uongozi Prof.Marcelina Chijoriga kwa kuwapokea wanafunzi na kuwapa ushirikiano mzuri kuanzia siku ya ufunguzi mpaka tamati ya mafunzo hayo.

Naye Rasi wa Shule Kuu ya Uongozi amesema "UDOM imeweka historia katika Shule Kuu ya Uongozi ya Kimataifa kwa kuwa Chuo cha kwanza kupeleka viongozi wa Serikali ya Wanafunzi kujifunza Uongozi na historia ya viongozi wetu mashuhuri.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo- Mpango Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson amewapongeza viongozi kwa kumaliza mafunzo hayo na kusema "mnaenda kuweka chuo chetu kwenye mazingira mazuri kupitia mafunzo haya na viongozi wote mkazungumze lugha ya aina moja katika utendaji" pia alitoa pongezi kwa wawezeshaji wa mafunzo haya ya uongozi kwa kazi nzuri waliofanya ya kuwajenga vijana.

Comments
Send a Comment