UNITE PARLIAMENTARIANS WAVUTIWA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA


  • 1 year
  • Office of The Vice Chancellor

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), umeanza mazungumzo na Shirika lisilokuwa la kiserikali la UNITE Parliamentarians Network for Global Health ili kuanzisha ushirikiano wenye lengo la kuleta mapinduzi katika huduma za afya kupitia maendeleo ya kidigitali.

Akizungumza wakati akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Bi. Bi. Eleonor Silva, Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Lughano Kusiluka amesema, wamefarijika sana na ujio na Bi. Eleonor na kwamba ni hamasa kubwa kuhusu ushirikiano huu ambao unalenga kutekeleza miradi ya maendeleo ya kina inayohusu afya ya kidigitali na teknolojia mpya inayotumia akili bandia (AI). Amesema, Lengo kuu la ushirikiano utakaoanzishwa ni kukabiliana na changamoto kubwa za afya ya umma ya kidigitali na kujenga daraja kati ya maendeleo ya kisayansi na watoa maamuzi.

Akiwa pamoja na Prof. Razack Lokina (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo wa Masuala ya Kitaaluma, Utafiti na Ushauri) na Prof. Wineaster Anderson (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo wa Mpango, Fedha, na Utawala), walionyesha Kwa kufanikisha hili, ushirikiano huo utatoa mafunzo na programu za kuimarisha uwezo kwa wadau, ikiwa ni pamoja na wabunge nchini Tanzania na maeneo mengine.

Shirika la UNITE Parliamentarians Network for Global Health, lenye makao yake makuu huko Lisbon, Ureno, linajulikana kwa azma yake thabiti ya kuboresha mifumo ya afya ulimwenguni kupitia sera madhubuti na endelevu. Baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nchi kama vile Kenya, Botswana, Mexico, Zimbabwe, na Argentina, sasa shirika hili limeelekeza nguvu zake kuelekea Tanzania kama hatua inayofuata.

Akizungumza, Bi. Eleonor Silva amesisitiza umuhimu wa kuanzisha uhusiano imara na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali, na kwamba anatazamia siku zijazo kuona sera zenye ufanisi na endelevu zitakuwa nguzo ya mifumo ya afya ya Tanzania.

Katika sehemu ya ziara yake, Bi. Silva pia alipata fursa ya kutembelea maonyesho yanayoendelea ya Wiki ya Ubunifu na Utafiti UDOM na kufurahishwa na ubunifu mkubwa ulioonyeshwa wa wafanyakazi na wanafunzi kutoka fani mbalimbali za Chuo hicho.
 

Comments
Send a Comment