UDOM KUWEZESHA UTALII WA KIMATIBABU TANZANIA
Chuo kikuu cha Dodoma kinatarajia kuifanya Tanzania kuwa eneo la utalii wa kimatibabu. Hayo yamesemwa tarehe 19 mwezi oktoba, 2023 na makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Prof Lughano Kusiluka alipokuwa akiwakaribisha wawakilishi wa taasisi na mashirika mbalimbali toka nchini Japani waliokuja kwa lengo la kufanya uwekezaji.
Akizungumza na wawakilishi hao, Prof Kusiluka amesema kwamba UDOM inataka kuleta utalii wa kimatibabu nchini kupitia uwezeshaji na usimamizi wa tafiti mbalimbali za kiafya kupitia watumishi wake wa kitaaluma.
Prof Kusiluka amesema kuwa, ili kuwezesha hilo, anawakaribisha wawakilishi hao toka nchini Japani kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya tafiti na huduma kwenye kada ya afya,ili kuletea matokeo Chanya.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, kiongozi wa msafara huo, naibu mkurugenzi ofisi inayoshughulika na sera za huduma za afya,baraza la sekretarieti ya Japani,Bi.Tomomi Sakurai amesema,nchi yake ilisaini makubaliano ya mashirikiano(MoU) mwaka jana ili kufanya ushirikiano na uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za afya,ambapo amesema kuwa ushirikiano huo utaleta tija na kuwezesha kuboresha huduma za afya nchini na tafiti za afya vyuoni.
“Japani inalengo la kupanua ushirikiano wake kimataifa kwa kuwezesha tafiti mbalimbali za kimatibabu kwa kuangalia changamoto mbalimbali za kiafya” ameongeza
Uwakilishi huo ulitoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo vyuo, hospitali na ofisi za serikali ya Japani.