WAFANYAKAZI WAHAMASISHWA KUFANYA MAZOEZI MARA KWA MARA KWA AJILI YA KUIMARISHA AFYA ZAO KATIKA KULETA UFANISI KAZINI
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi THTU tawi la Chuo kikuu cha Dodoma Ndg.Edson Baradyana amewataka wafanyakazi kuweka desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya zao na kuleta ufanisi kazini.
Rai hiyo ilitolewa wakati akifungua BONANZA la Wafanyakazi maarufu kama *MTANI JEMBE* lililowakutanisha wafanyakazi mashabiki wa Simba na Yanga, wakichuana katika Michezo liliyoandaliwa na Chama hicho kama sehemu ya sherehe ya wafanyakazi maarufu kama MCHAPALO tarehe 19 Oktoba, 2023 katika viwanja vya Ndaki ya Komputya na Elimu Angavu ( CIVE GROUND).
Michezo mbalimbali ilifanyika ikiwemo Mpira wa Miguu,Mpira waPete,Riadha,Bao,Draft,Karata na Darts