UDOM YAIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA KIMATAIFA LA USALAMA NA ULINZI WA MTANDAO


  • 1 year
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kimeibuka mshindi wa Pili katika shindano la kimataifa la usalama na ulinzi wa mtandao (Cyberlympics Competition 2023) yaliyoratibiwa nchini Rwanda kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2023 na washindi kutangazwa tarehe 4 Novemba, 2023.

Shindano hilo ambalo kwa Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma pekee kilipata nafasi ya kuwakilisha Taifa, na kuibuka na ushindi mkubwa likijumuisha washiriki kutoka nchi 54 barani Afrika.

Wanafunzi walioshiriki katika shindano hili walijulikana kwa jina la timu TCTForce, ambao ni Peter Lyimo - Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Programu, Baraka Range - Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Programu na David Olendukai - Mwanafunzi wa Sayansi katika Uhandisi wa Kompyuta.

Aidha, washindi wa tatu ambao pia ni kutoka UDOM wakijulikana kwa jina la timu Alexius ni Alexius Samson- Mwanafunzi wa Shahada Sayansi katika Usalama wa Mtandao na Uhandisi wa Uchunguzi wa Kidijitali, Bw.Mpotisambo Zamea- Mwanafunzi wa Shahada Sayansi katika Usalama wa Mtandao na Uhandisi wa Uchunguzi wa Kidijitali , Bw. Erick Alex - Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Mitandao ya Kompyuta na Uhandisi wa Usalama wa Habari na Bw.Ally Riadha- Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Mitandao ya Kompyuta na Uhandisi wa Usalama wa Habari.

Shindano hili hufanyika kila mwaka ambapo lengo lake kubwa ni kushughulikia tatizo la usalama wa mtandao na mgawanyiko wa kidigitali ambao unaendelea barani Afrika. Nia ya mashindano hayo ni kuifanya Afrika kuwa kitovu cha Teknolojia.

Pongezi kwa Wanafunzi saba (7) kutoka Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu kwa kupeperusha vyema bendera ya UDOM na Tanzania.
 

Comments
Send a Comment