MRADI WA HEET UDOM WAWEZESHA UHAMASISHAJI MASOMO YA SAYANSI KWA WATOTO WA KIKE


  • 1 month
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia mradi WA HEET kipo kwenye program ya uhamasishaji wanafunzi wa kike waliopo Shule za Sekondari na Shule za Msingi ili waweze kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi.

Uhamasishaji huu unalenga kuondoa dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kwamba masomo ya Sayansi ni magumu na kwamba yanaweza kusomwa na watoto wa kiume zaidi kuliko wa Kike.

Licha ya uhamasishaji huo, program hii ina lengo la kuzitangaza programu mbalimbali zinazotolewa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa ngazi ya Shahada ya Awali katika taaluma za STUH (yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati) katika Ndaki za Sayansi Asilia na Hisabati, Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi, Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa, pamoja Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii.

Program hii inafanyika katika mikoa ya Kigoma, Geita, Simiyu, Lindi, Mbeya, Songwe na Pwani na katika Mkoa wa Kigoma. Shule ambazo tayari zimetembelewa ni Sekondari ya Mwananchi, Shule ya Sekondari Bulonge, Shule ya Msingi Uhuru, Muungano, Alpha Primary School na Bright Star Academy

Comments
Send a Comment