UDOM YANG`ARA TUZO ZA HUAWEI
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimenga’ra kwa kutoa washindi watano katika tuzo za programu ya kuinua vipaji katika maendeleo ya teknolojia kwa vijana ijulikanayo kama (HUAWEI SEEDS FOR THE FUTURE) zinazotolewa na Taasisi ya vifaa vya kielektroniki ya HUAWEI.
Wanafunzi hao watano waliopata tuzo hizo ni miongoni mwa wanafunzi kumi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma walioshiriki katika program hiyo na kupata tuzo ya utambuzi iliotolewa tarehe 18 Disemba 2023 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Waziri wa Habari na Teknolojia Mhe. Nape Nnauye amesema Program hii ina lengo la kuinua na kuwezesha vijana kujenga mustakabali wa kidigitali na kuleta maendeleo ya nchi kiujumla.
Mhe. Nape pia ameipongeza kampuni ya HUAWEI kwa kuwezesha program hiyo inayowasaidia vijana walioko vyuoni kushiriki katika mafunzo ya teknolojia na kidigitali.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof Lughano Kusiluka amesema kuwa anatambua na anapongeza mchango wa kampuni ya HUAWEI kwa kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana katika nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini na duniani kwa ujumla.
Chuo Kikuu cha Dodoma kimeshiriki katika programu hii toka mwaka 2016 na kwa mwaka 2023 UDOM ilitoa washiriki kumi na kati ya hao watano wamefanikiwa kutunukiwa vyeti na kutambulika rasmi katika Programu ya HUWAWEI Seeds for the Future