MAAFISA MAWASILIANO NA WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUWEKEZA KWENYE MAWASILIANO YA KISAYANSI


  • 4 days
  • The University of Dodoma

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka amewasilisha mada kuhusu Mawasiliano ya kisayansi “ Science Communication” akiwataka Maafisa Mawasiliano na Waandishi wa habari kuongeza juhudi kuandika habari na matokeo ya tafiti za kisayansi kwa maendeleo mapana ya Afrika.

Amesema, kufuatia mabadiliko ya Nne ya Kiuchumi duniani yanayoendana na uwekezaji Mkubwa katika ubunifu wa kisayansi, Vyombo vya habari na Maafisa Mawasiliano wanaowajibu mkubwa wa kusaidia Afrika na hasa Afrika Mashariki, kuandika matokeo ya utafiti na bunifu za kisayansi zinazofanywa na wanasayansi, ili kuongeza uelewa wa wananchi katika masuala ya Sayansi na kuongeza ushiriki wao katika kuleta mabadiliko chanya.

Amehidi Chuo Kikuu cha Dodoma, kuanzisha mafunzo ya muda mfupi yatakayosaidia waandishi na Maafisa Habari kuandika habari za kisayansi kwa manufaa mapana ya Taifa.

Mkutano huo wa siku tano unahusisha washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Burundi, Rwanda na Sudan; na unajadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeo na Ustawi wa Tasnia ya Mawasiliano ya Umma na Mawasiliano.

Comments
Send a Comment