UDOM KUSHIRIKIANA NA INDIA KUBORESHA ELIMU


  • 4 weeks
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na serikali ya India wamekubaliana kushirikiana katika kuhakikisha kwamba wanaboresha elimu inayotolewa kwa wanafunzi wa UDOM.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika UDOM Oktoba 4, 2024 Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Bishwadip Dey amesema serikali ya India inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kwenda nchini India kujifunza zaidi kuhusiana na maswala ya TEHAMA, Uchimbaji Madini na Famasia.

Mhe. Dey amesema India ina mpango wa kutoa ufadhili wa vitabu kwa wanafunzi wa UDOM pamoja na kuanzisha mpango wa kubadilishana tamaduni kati ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusilika amesema kupitia mashirikiano haya, wanafunzi watapata fursa ya kuwa wabobezi kwa vitendo katika fani za Sayansi na TEHAMA.

Chuo Kikuu cha Dodoma kimeendelea kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu ambayo inaenda kuwa suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika ulimwengu huu wa kidigitali.
 

Comments
Send a Comment