UDOM YAPONGEZWA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


  • 4 days
  • The University of Dodoma

Katika kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kuwa moja kati ya wateja bora wa shirika hilo.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza Chuo Kikuu cha Dodoma, Mwakilishi wa Meneja wa TANESCO Dodoma Bi. Monica Mabada amesema UDOM ni moja kati ya wateja bora na waaminifu ambao wamekuwa wakilipa bili kwa wakati. Aidha, alieleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya UDOM na TANESCO ambao umewezesha taasisi hizi mbili kufanya kazi kwa karibu wakati wowote.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika hafla hiyo Prof. Ismail Juma Ismail amesema kuwa, kwa muda mrefu UDOM wamekuwa ni wanufaika wakubwa wa nishati ya umeme kutoka TANESCO, hivyo amewaomba wazidi kuboresha huduma hii.

Umeme unaozalishwa na TANESCO ni moja kati ya nishati ambayo imekuwa ikitegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye matumizi ya kila siku ya uendeshaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
 

Comments
Send a Comment