HEET YAWEZESHA MAFUNZO YA UFUNDISHAJI KIDIGITALI UDOM


  • 1 day
  • The University of Dodoma

Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) umewezesha utoaji wa mafunzo ya ufundishaji kwa njia ya Mtandao kwa Wahadhiri na Wataalamu wa TEHAMA wa Chuo Kikuu cha Dodoma yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 15 Oktoba, 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi UDOM Prof. Ainory Peter Gesase amesema mafunzo haya ni muhimu sana na yanahitajika kwenye ulimwengu huu wa kijigitali kwa ajili ya kurahisisha njia za utoaji na upatikanaji wa elimu.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi kutoka Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu UDOM Dkt. Lucian Ngeze amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha wahadhiri kuweza kufundisha masomo yote kwa njia ya mtandao.

Naye, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Idara ya Jiografia na Stadi za Mazingira katika Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii (UDOM) Dkt. Mohamed Khamis Said amesema baadhi ya faida za mafunzo haya ni pamoja na kumwezesha mwanafunzi kujifunza hata anapokuwa nje ya eneo la chuo. Pia, ameomba mafunzo ambayo yatakuwa yakitolewa mtandaoni yawe rafiki kwa watu wenye mahitaji maalum kama vile watu wasiona na kusikia.

Mafunzo haya ni moja kati ya malengo ya utekelezaji wa Mradi wa HEET lengo likiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa elimu katika ulimwengu huu wa kidijitali.
 

Comments
Send a Comment