UDOM YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


  • 2 days
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Shule Kuu ya Sheria kimeadhimisha siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kongamano hilo lilihusisha wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Chuo.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika tarehe 10 Oktoba 2024 Kaimu Amidi wa Shule Kuu Dkt. Elia Mwaga amesema kuanzia tarehe 25 Oktoba 2024 Shule Kuu ya Sheria ilianza maadhimisho hayo kwa kufanya programu mbalimbali za Kuelimisha jamii kuhusiana na Ukatili wa Kijinsia ambapo ziliambatana na mbinu mbalimbali katika kufikia idadi kubwa ya watu kama Midahalo, Michezo, Matembezi, Maandamano ya amani na kutoa msaada wa Kisheria

"Ukatili wa Kijinsia ni tatizo la Dunia na kwa Tanzania wapo waathirika wengi ambao wanakumbwa na ukatili wa kijinsia lakini kibaya zaidi watu ambao wanakumbwa na ukatili wa Kijinsia wamekuwa hawatoi taarifa kwenye mamlaka husika ili hatua Stahiki ziweze kuchukuliwa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua kupinga Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na kuwasaidia na kutoa taarifa kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia; Aliongeza Dkt. Mwaga

Kwa upande wa Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya Upatikanaji wa Haki GIZ-Tanzania
Bw. Brahimi Muhamet, amesema kama Shirika la GIZ wamekuwa wanafanya Programu nyingi na wanafunzi wa Shule Kuu ya Sheria wakiamini kwamba ndo kizazi cha baadae cha kuleta Maendeleo kwa Taifa na amefurahia kuwa kile walichokianzisha mwaka jana kinaendelea kufanyika na ameahidi kuwa kama Shirika wataendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma

Naye; Mwanafunzi wa Shule Kuu ya Sheria Mwaka wa Nne Bi. Neema Ochola amesema kwa mwaka huu wanafunzi wa kiume wamekuwa na mwamko zaidi katika kuhamisha kutokemeza vitendo vya ukatili wa Kijinsia

Comments
Send a Comment