UDOM YANG`ARA TUZO ZA UANDAAJI BORA WA HESABU


  • 3 days
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kimeibuka Mshindi wa Tatu katika kundi la Taasisi za Elimu ya Juu kwa uandaaji wa Hesabu bora kwa mwaka 2023.

Mafanikio hayo yanatokana na uandaaji bora wa hesabu za Taasisi kwa mwaka 2023 kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji Hesabu kwa Taasisi za Umma (IPSASs) ambapo Tuzo hizo huandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

Tuzo hizi zimetolewa tarehe 29 Novemba 2024 katika viwanja vya APC Bunju Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Taasisi Mbalimbali za Serikali.

Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (IAG), Ndg. Benjamin Mashauri Magai.
 

Comments
Send a Comment