UDOM KUSHIRIKI MASHINDANO KENYA
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Razack Lokina, leo tarehe 13 Desemba, 2024 amewaaga Wanafunzi 57 ambao wanatarajia kushiriki Mashindano ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki ambayo kwa mwaka huu yanafanyika Kisumu nchini Kenya, kuanzia tarehe 14 hadi 21 Desemba 2024.
Prof. Razack Lokina amewataka Wanafunzi hao pindi watakapokuwa kwenye Mashindano hayo wazingatie nidhamu na kurudi na ushindi kama ilivyo desturi ya UDOM.
" Msirudi mikono mitupu mpambane, ndo maana tumewapatia mahitaji yote mnayohitaji; tukatangaze nchi yetu maana mmeshikilia bendera mbili ya Taifa na UDOM". Alisisitiza
Naye Mkufunzi wa Michezo Bw. Deogratius Mdemu, amesema michezo inayokwenda kushindaniwa ni Mpira wa Miguu wanawake na wanaume, mpira wa Wavu, Mpira wa Pete na mchezo wa Walemavu “Mpira wa Wasioona “Goal ball”