CHUO KIKUU CHA DODOMA KINASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU TANGA


  • 1 month
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeendelea kuwa kivutio kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Elimu Tanga, yanayoendelea sambamba na maonesho ya Elimu, Ubunifu na Teknolojia, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal, Bombo.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la UDOM wamefurahishwa na Ubunifu mkubwa uliofanywa na wanafunzi kupitia bidhaa zao, ikiwemo dawa ya asili inayodhaniwa kutibu ugonjwa wa kisukari. Bidhaa nyingine za ubunifu ni Mfumo unaosaidia kutatua athari za mazingira na utupaji taka ovyo, mfumo wa kidigitali unaorahisisha urinaji asali, utengenezaji wa mifuko mbadala ya plastiki kwa kutumia zao la mwani, dawa ya asili ya kutibu malaria na ugonjwa sugu wa U.T.I kwa akina mama wajawazito na uchoraji kisanifu.

Huduma zingine zinazotolewa ni ushauri bure kwa wanafunzi waliomaliza shule na wanataka kujiunga na UDOM kwa masomo ya Elimu ya Juu, pamoja na kuendelea kuwaongezea wananchi wa Tanga uelewa zaidi huku shughuli za Chuo Kikuu cha Dodoma katika ufindishaji, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma.

Comments
Send a Comment