WAZIRI MKUU AVUTIWA NA UBUNIFU UDOM


  • 3 weeks
  • The University of Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amevutiwa na ubunifu uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.

Akizungumza wakati alipotembelea Banda la UDOM katika Kilele cha Maadhimisho hayo tarehe 31 Mei, 2024, Mhe. Majaliwa amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuweza kubuni vifungashio mbadala ambavyo ni rafiki kwa Mazingira.

Aidha, ametoa wito kwa UDOM kuendelea kufanya tafiti na kuja na bunifu nyingi za kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, likiwemo suala la vijana kujiajiri.

Naye, mbunifu wa vifungashio hivyo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma ambaye ni Mkufunzi Msaidizi Bw. Mohammed Amini, kutoka Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati (CNMS) amesema vifungashio hivyo vinatengenezwa kwa malighafi taka na zao la mwani na hivyo gharama za kuzalisha ni ndogo kiasi cha kila mwananchi kuzimudu.

Comments
Send a Comment