UDOM WATOA MAFUNZO YA SARATANI YA MACHO GEITA


  • 5 months
  • The University of Dodoma

Wataalamu wa tiba za binadamu toka Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Shirika la Kimarekani la Conquer Cancer wametoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wa kitengo cha kliniki ya mama na mtoto mkoani Geita

Mafunzo hayo yaliyolenga upimaji na utambuzi wa saratani ya macho kwa watoto yalifanyika kwa siku tatu kuanzia tar 1-3 Agosti 2024 Mkoani Geita yalihusisha watoa huduma 40 katika kliniki 10, kwa kuwapatia vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ya upimaji wa macho kwa watoto.

Katika Wilaya ya Sengerema mafunzo yalifanyika kwa wahudumu zaidi ya 40. Aidha, wataalamu walifanya tathimini juu ya mafunzo yaliyotolewa katika Wilaya hiyo miezi 8 iliyopita yalivyosaidia na changamoto walizopitia

Washiriki wa mafunzo hayo wamewashukuru watalaamu kutoka UDOM kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani awali walikuwa na changamoto kubwa ya uelewa mdogo wa watoa huduma ngazi ya msingi kuhusu saratani ya macho kwa watoto.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwenye kila wilaya
moja katika mikoa mitatu inayoripotiwa kuwa na watoto wengi wenye saratani ya macho ambayo ni Mwanza, Geita na lringa.

Comments
Send a Comment