UJUMBE TOKA BENKI YA DUNIA NA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA WATEMBELEA MRADI WA HEET UDOM
Ujumbe kutoka Benki ya Dunia pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma tarehe 9 Aprili, 2025, kukagua maendeleo ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Ujumbe huo ulitembelea Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi pamoja na Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati, ambako ujenzi wa majengo ya madarasa na Maabara unaendelea.
Ujumbe huo umehimiza Menejimenti kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha kazi ndani ya muda uliowekwa na kuheshimu makubaliano ya Mkataba kwa ubora unaostahili.