WANAFUNZI WANNE KUIWAKILISHA UDOM KIMATAIFA
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu (CIVE), leo tarehe 16 Mei, 2025 kimefanya hafla fupi ya kuwakabidhi bendera wanafunzi wanne (4) Sigfrid Michael, Paul Nkingwa, Godlove Hipolite na Felix Kuluchumila, wanaokwenda nchini China kuliwakilisha Tanzania kwenye Fainali ya Mashindano kidunia (Huawei ICT Competition).
Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu(CIVE) imekuwa ikipeperusha vyema bendera ya (UDOM) kwenye mashindano mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ndani na nje ya nchi.
Makabidhiano hayo yalifanywa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka ambaye aliwapongeza na kuwapa motisha ya kurudi na ushindi.