WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA NCHINI CANADA ATEMBELEA UDOM


  • 1 day
  • The University of Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Randeep Sarai amefanya ziara ya kutembelea na kukutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Jumatatu tarehe 21 Julai, 2025. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kujadili juu ya mradi matumizi ya Akili Unde (AI) katika Maendeleo unaofadhiliwa na Serikali ya Kanada kupitia Taasisi ya International Development Research Centre (IDRC).

Katika ziara hiyo Mhe. Sarai ameupongeza Uongozi wa UDOM kwa kutimiza kikamilifu lengo kuu la mradi kwa kujenga Maabara inayowezesha kuimarisha uwezo wa wanataaluma kufanya tafiti za matumizi ya Akili Unde (AI) na kuwajengea uwezo watafiti wachanga katika kubaini changamoto za kiafya kwa kutumia Akili Unde.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano kusiluka ameishukuru Serikali ya Kanada kwa kufadhili miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Chuo Kikuu cha Dodoma na kuahidi kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Katika ziara hiyo Mhe. Sarai aliambatana na Balozi wa Kanada nchini Tanzania Mhe. Emily Burns, wadau wa maendeleo kutoka Global Affairs Canada (GAC) na IDRC, Watafiti kutoka Taasisi ya Sayansi. na Teknolojia ya Nelson Mandela Uongozi na watekelezaji wa mradi kutoka UDOM.

Comments
Send a Comment