CPA MWAKAPALA AFANIKIWA KUTETEA TASNIFU YA UZAMIVU


  • 5 days
  • The University of Dodoma

Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu "PhD" kutoka Ndaki ya Biashara na Uchumi CPA. David Mwakapala amefanikiwa kutetea Tasnifu yake ya shahada ya Uzamivu kuhusu Umuhimu wa Uzingatiaji Viwango vya Kimataifa katika Uandaaji wa Hesabu za Vyama vya Ushirika, Akiba na Mikopo Tanzania.

Baada ya kuwasilisha matokeo ya tafiti yake mbele ya jopo la wasimamizi CPA. Mwakapala ametakiwa kufanya marekebisho madogo ili kukamilisha tasnifu yake.

Uwasilishaji wa matokeo ya tafiti hiyo umefanyika tarehe 10 Januari 2025 katika
Ukumbi wa CIVE- New Computer Lab Postgraduate Lab No.2 huku wengine wakifuatilia kwa njia ya mtandao.

CPA. Mwakapala ameshukuru wasimamizi wake pamoja na wote walimsadia kufanikisha safari yake ya shahada ya Uzamivu. Aidha, alieleza kuwa safari hiyo imemchukia miaka minne kuikamilisha.

Naye, Msimamizi wa Mwanafunzi huyo Dkt. Sarah Ngomuo amempongeza CPA Mwakapala kwa uwasilishaji mzuri wa tafiti yake huku akieleza kuwa watafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na jopo la wasimamizi ili kuboresha utafiti huo.

Comments
Send a Comment