UDOM YATOA MAFUNZO YA ITIFAKI NA USTARAABU
Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii ( CHSS) kimeanza kutoa mafunzo mafupi juu ya misingi ya Weledi Itifaki na Ustaraabu kuanzia leo tarehe 28- 31 Januari, 2025.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo katia Ukumbi wa Mikutano ( CHSS) Rasi wa Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii Prof. Albino Tenge amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwasadia Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kuwajengea ujuzi na kuwaongezea maarifa mapya ambayo yanahitajika kwa kuwa kila siku mambo yanabadilika
" Niwashukuru kwa Kuchagua kuja kupata mafunzo haya Chuo Kikuu cha Dodoma, tunashukuru kwa kutupa heshima hiyo, tuna imani kwamba baada ya kumaliza mafunzo haya mtatoka na kitu ambacho kitakuwa kimeongezeka katika kutekeleza majukumu yenu hususani katika weledi, Itifaki na Ustaraabu". Aliongeza Prof. Tenge
Naye; Mkuu wa Idara, Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma ( CHSS) Dkt. Parestico Pastory amesema wamefanikiwa kupata washiriki 25 kutoka Tanzania bara na visiwani na alisisitiza kuwa kupitia Idara hiyo wataendelea kutoa mafunzo kila baada ya muda fulani kwa kuwa wana Programu Maalumu ya mafunzo ya uongozi ili kuendelea kuimarisha ujuzi kwa watumishi wa Serikali na Sekta Binafsi ikiwa ni mojawapo la jukumu la Chuo kutoa huduma kwa jamii