UDOM KUANZISHA PROGRAMU MAALUMU YA UTHIBITISHO UBORA KWA WATAALAMU WA TEHAMA
Chuo Kikuu cha Dodoma kiko mbioni kuanzisha programu ya mafunzo ya Uthibitisho wa Ubora wa Wataalam wa Usalama Mtandaoni (Cybersecurity Professional Certification Program), hatua ambayo ni muhimu kuelekea kuboresha elimu na mafunzo ya usalama wa mtandao, inayotolewa na Chuo Kikuu cha Dodoma, pamoja na kuongeza wigo wa ajira kwa wataalamu wanaozalishwa nchini.
Hayo yameelezwa leo Jumatano tarehe 05 Februari 2024, na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, alipokutana na kufanya mazungumzo na Bw. Edward Sundberg, Mratibu wa programu ya mafunzo kwa Afrika kutoka Shirika la Africa Program for Cyber Technology (APCT).
Akizungumzia Programu hiyo, Bw. Edward amesema, mafunzo hayo yatatolewa kwa miezi sita kwa njia ya mtandao, kwa kuanza na kundi la wanafunzi 200, kwa usimamizi wa wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Ngavu ( CIVE]) kwa ushirikiano na Washirika wa programu hiyo waliopo nchini Marekani.
Aidha, kabla ya kupaya cheti, wanafunzi wote watafanya mitihani ambayo itaandaliwa kwa lengo la kuthibitisha ubora.