UDOM KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUZALISHA WATALAAMU WA TEHAMA
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Razack Lokina, amesema Chuo Kikuu cha Dodoma, kimejizatiti katika kutekeleza maagizo ya Serikali ya kuzalisha wataalamu wabobevu kwenye sekta ya TEHAMA, pamoja na kuendelea kushirikiana na Serikali kufanya Utafiti hususani katika maeneo yanayohusu udhibiti wa usalama, usalama wa taarifa mtandaoni pamoja na kusaidia kuunganisha mifumo ya Serikali kusomana taarifa.
Hayo ameyasema Jumanne tarehe 11 Februari 2025, wakati akishiriki Kikao Kazi cha Tano (5) cha Serikali Mtandao (e-GA), akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo.
“Kama unavyoona UDOM imedhamini na imeshiriki kwenye Mkutano huu mkubwa kitaifa, na tumekuja na bunifu kwenye teknolojia Mnembe, ili kudhihirishia watanzania kwamba tumejizatiti katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kwa kutumia teknolojia” alisema
Prof. Razack amesema, UDOM imeendelea kufanya vizuri katika ufundishaji na kuwa miongoni mwa vyuo bora vinavyozalisha wataalamu wa TEHAMA, na kupitia mashindano mbalimbali yanayofanyika kitaifa na kimataifa, UDOM imeendelea kuwa kinara ikionyesha ubobevu wa wataalamu wake katika kuzalisha wataalamu wenye ubora na weledi hasa katika masuala yanayohusu usalama wa mitandao.
Mkutano wa Tano wa Serikali Mtandao, ulizinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza e-GA kuendelea kushirikiana na Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini katika kuhakikisha malengo ya Serikali Mtandao yanafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuzalisha wataalamu wa ndani kusaidia jitihada za Serikali za kuwa na udhibiti wa vitisho vya usalama wa taarifa, na vitisho vya usalama mtandaoni.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Razack Lokina, amesema Chuo Kikuu cha Dodoma, kimejizatiti katika kutekeleza maagizo ya Serikali ya kuzalisha wataalamu wabobevu kwenye sekta ya TEHAMA, pamoja na kuendelea kushirikiana na Serikali kufanya Utafiti hususani katika maeneo yanayohusu udhibiti wa usalama, usalama wa taarifa mtandaoni pamoja na kusaidia kuunganisha mifumo ya Serikali kusomana taarifa.
Hayo ameyasema Jumanne tarehe 11 Februari 2025, wakati akishiriki Kikao Kazi cha Tano (5) cha Serikali Mtandao (e-GA), akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo.
“Kama unavyoona UDOM imedhamini na imeshiriki kwenye Mkutano huu mkubwa kitaifa, na tumekuja na bunifu kwenye teknolojia Mnembe, ili kudhihirishia watanzania kwamba tumejizatiti katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kwa kutumia teknolojia” alisema
Prof. Razack amesema, UDOM imeendelea kufanya vizuri katika ufundishaji na kuwa miongoni mwa vyuo bora vinavyozalisha wataalamu wa TEHAMA, na kupitia mashindano mbalimbali yanayofanyika kitaifa na kimataifa, UDOM imeendelea kuwa kinara ikionyesha ubobevu wa wataalamu wake katika kuzalisha wataalamu wenye ubora na weledi hasa katika masuala yanayohusu usalama wa mitandao.
Mkutano wa Tano wa Serikali Mtandao, ulizinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza e-GA kuendelea kushirikiana na Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini katika kuhakikisha malengo ya Serikali Mtandao yanafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuzalisha wataalamu wa ndani kusaidia jitihada za Serikali za kuwa na udhibiti wa vitisho vya usalama wa taarifa, na vitisho vya usalama mtandaoni.