MKUU WA CHUO UDOM AKUTANA NA MENEJIMENTI


  • 21 hours
  • The University of Dodoma

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, leo tarehe 24 Februari 2025 ametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma, na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo.

Mhe. Stergomena alipokelewa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Bi. Suzan P. Mlawi, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma Prof. Razack Lokina na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Winester Anderson.

Mhe. Stergomena Tax amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Menejimenti ya Chuo katika kusimamia ubora wa taaluma, kutunza taswira ya chuo na kuweka msisitizo wa kuendelea kutatua changamoto zote kwa wakati, husani zile zinazohusiana na maendeleo ya wanafunzi.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, akimkaribisha Mkuu wa Chuo, amemwelezea mikakati ya namna Menejimenti ilivyojipanga kuendelea kusimamia ubora wa taaluma inayotolewa na Chuo, pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa masuala ambayo yanahitaji ufafanuzi kwa jamii.

Comments
Send a Comment