BARAZA LA CHUO KIKUU CHA DODOMA LAPATIWA MAFUNZO YA UTAWALA BORA


  • 1 week
  • The University of Dodoma

Baraza za Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 03 Machi lilianza mafunzo ya siku tatu ya Uongozi na uendeshaji bora wa Taasisi, yanayofanyika mkoani Arusha katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC, kwa usimamizi wa Taasisi ya Uongozi.

Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Rwekaza Sympho Mukandala, amewataka wajumbe na Menejimenti kuwa makini katika mafunzo hayo ili yasaidie kuongeza ufanisi, utendaji kazi na kuleta tija kwa Baraza la Chuo, katika kuisimamia Menejimenti katika masuala yote yanayohusu maendeleo na ustawi wa Chuo.

Miongoni mwa mambo yanayofundishwa ni Utawala bora wa Taasisi na Ustadi wa Viongozi, Changamoto zinazoendelea katika Utawala Bora na uelewa wa Masuala ya Kifedha, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Kimkakati wa Rasilimali za Umma, Usimamizi wa Mashirika na Usimamizi wa Vihatarishi.
 

Comments
Send a Comment